News Posts
GARI LA WOLPER...
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 7:29am 0 Comments 0 Likes
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ‘mchuma’ huo ambao ‘umetaitiwa’ na Kampuni ya Udalali ya Majembe ya jijini Dar es Salaam kwenye yadi yao ya Mikocheni, umekuwa ukipata wateja kila kukicha ambao wanakwenda kuulizia siku ya mnada.
Chanzo kingine kilisema kuwa mbali na wateja kumiminika yadi ya Majembe, kumekuwa na usumbufu mwingi kwenye ofisi za TRA, Posta jijini Dar ambapo baadhi ya matajiri nao wamekuwa wakilifukuzia gari hilo kwa lengo la kulinunua.…
KATUNI MIX...
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 9:07am 0 Comments 0 Likes
SYLVIA SHALLY, KOLETA WADAIWA MAWIGI
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 7:29am 0 Comments 0 Likes
Sakata hilo la aina yake limeibuliwa hivi karibuni ambapo Flora Mwande maarufu kwa jina la ‘Gari Kubwa’ mkazi wa Mbagala, Dar alisema anawadai kwa muda mrefu mastaa hao fedha za bidhaa mbalimbali yakiwemo mawigi.
Gari Kubwa alisema kuwa yeye ndiye anayewapendezesha mastaa hao kwa kuwakopesha nywele, pete, cheni na vitu vingine vya kike vyenye mvuto lakini mwisho wanampiga chenga kulipa fedha zake na kuingia mitini, jambo ambalo alidai limekuwa likimrudisha nyuma kimaendeleo.
“Sylvia alikuja dukani kwangu, Sayansi, Kijitonyama (Dar) Februari 17, 2011 akakopa nywele akisema yuko kwenye maandalizi ya kwenda nchini Nigeria. Alichukua ‘lesi wigi’…
MAWAZO HUCHANGIA UGUMBA KWA WANAWAKE
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 8:58am 0 Comments 0 Likes
Aina hii ya homoni ndiyo inayosimamisha mchakato wa uzalishaji wa mayai kwa wanawake wanaoshiriki mchezo wa riadha.
Hivyo basi, uwiano huu wa kasoro za ukuzaji mayai kati ya wakimbia riadha na wanawake wagumba unaweka usawa baina ya uchovu mkubwa wa mazoezi ya viungo na ule uchovu unaotokana na msongo wa mawazo ya ugumba.
Ukweli pekee ambao nimeukusudia kuuzungumza leo ni kuhusiana na wanawake wasiokuwa na matatizo ya uzazi ambao utafiti ulioandikwa katika jarida la Minerva Ginecologica la nchini Italia unaonesha mawazo ndiyo unaochangia kwa kiasi kikubwa wanawake hao wasipate watoto licha ya kwamba kibaiolojia hawana matatizo.
Imebainika kuwa,…
UZINDUZI WA SKYLIGHT BENDI ULIVYOBAMBA NDANI YA GIRAFFE OCEAN VIEW, DAR
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 8:45am 0 Comments 0 Likes
BAHATI BUKUKU NUSURA APEWE TALAKA BAA
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 7:27am 0 Comments 0 Likes
STAA wa nyimbo za Injili Bongo anayetamba na albamu ya Dunia Haina Huruma, Bahati Bukuku amenusurika kulimwa talaka baa kutoka kwa mumewe waliyetengana naye miaka 7 iliyopita, Daniel Basila.
Kwa mujibu wa chanzo, ishu hiyo ilitokea mwishoni mwa mwezi Julai, mwaka huu ndani ya Baa ya Land Mark Hotel iliyopo Ubungo, jijini Dar.
Ilidaiwa kuwa, Basila alimwita ‘mtalaka’ wake huyo hotelini hapo ampe talaka yake baada ya kuishi ‘singo’ kwa miaka saba huku ndoa yao ikiwa haijulikani hatima yake.
“Daniel alimwita Bahati kwa simu, akamwambia aende pale hotelini akampe talaka. Alipofika alimkuta jamaa ameshika kikaratasi eti ndiyo talaka, lakini Bahati akamwambia kama amedhamiria kutoa talaka aende mahakamani,” kilisema chanzo.…

JULIET AGEUKIA FILAMU
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 7:27am 0 Comments 0 Likes
MISS Progress International 2010, Juliet William amegeukia sanaa ya uigizaji baada ya kumaliza mradi aliokuwa akiufanya wa kuwasaidia walemavu wa ngozi (albino).
Akichonga na Motomoto Newz, Juliet alisema ameamua kuingia kwa asilimia mia moja kwenye gemu la uigizaji kwa vile amegundua ndiyo fani inayolipa hasa akizingatia kuwa ana kipaji.
Alisema kwa kuanzia anaandaa filamu yake inayokwenda kwa jina la Sister Juliet aliyomshirikisha Sylvia Shally.
“Nimeamua kujikita katika filamu kwa sasa, mradi wa kusaidia walemavu wa ngozi nitaendelea nao baadaye. Kwa kuanzia nimeandaa filamu yangu ya Sister Juliet nikicheza na Sylvia Shally,” alisema…

MATUKIO AANZA MAANDALIZI YA KUTEMBEA KWA MIGUU DAR MPAKA MORO
Posted by GLOBAL on August 23, 2012 at 7:26am 0 Comments 0 Likes
MWANAHARAKATI wa Bongo aliye pia Mr. University 2002, Matukio Chuma ameanza maandalizi ya matembezi yake ya kutoka Dar mpaka Morogoro yenye lengo la kumhamasisha kila Mtanzania kujua nini anafanya kwa ajili ya nchi yake.
Julai 27, mwaka huu, mwanaharakati huyo alizindua mpango wake huo alipoongea na mapaparazi kwenye Kijiji cha Makumbusho, Dar na kusema anakaribisha watu kujiunga na zoezi hilo litakalofanyika Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na Motomoto Newz juzikati, Dar, Matukio alisema ameanza kupokea maombi ya watu kujiunga, pia ameanza mazoezi ya kujiweka fiti kwa ajili ya zoezi hili sanjari na kuratibu maeneo atakayopiga kambi akiwa njiani kwenda Moro. …

SABABU ZA WANAUME KUPENDA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA!
Posted by GLOBAL on August 22, 2012 at 10:00pm 0 Comments 0 Likes
Mada ambayo nataka kuizungumzia leo ni juu ya sababu za baadhi ya wanaume kupenda au kudatishwa kimahaba na wanawake wenye makalio makubwa.
Katika siku za hivi karibuni, tumeshuhudia idadi kubwa ya wanawake wakitumia njia mbalimbali kuhakikisha wanakuwa na makalio makubwa. Wapo ambao wamekuwa wakitumia dawa za Kichina licha ya kuelezwa kuwa zina madhara.
Ukijaribu kuzungumza nao, wengi wanasema wanatafuta soko kwa wanaume wakware. Wanaosema hivyo ukiwafuatilia ni wale ambao wamekaa kibiashara zaidi. Yaani wapo sokoni kuwinda wanaume.
Lakini sasa inafika…